Huku nchi ikiadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, Wakenya wamehimizwa kufanyiwa uchunguzi wa matiti mara kwa mara ili kugundua ugonjwa huo mapema. Wito huo ulitolewa wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika Kituo cha Saratani cha Texas, ambapo madaktari wakiongozwa na mtaalamu wa saratani Mumo Muoki walionyesha wasiwasi kwamba wagonjwa wengi hutafuta matibabu wakati saratani tayari imesambaa hivyo kupunguza chaguzi za matibabu zinazopatikana.

VOX POP-CANCER