Eliud Kipchoge aliendelea kuandika upya historia kuhusu ukuu wake baada ya kushinda Marathon nchini Australia. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 41 alitumia saa 2 dakika tisa kuweka rekodi mpya ya mbio katika tamasha la Nike huko Melbourne. Huenda Kipchoge angetumia muda wa kasi zaidi kama hangepunguza mwendo ili kuwatambua mashabiki alipokaribia mstari wa kumalizia. Baada ya kumaliza wa pili huko Cape Town, bingwa huyo mara mbili wa Olimpiki aliwashinda Thomas Do Canto na Reece Edwards wote wawili, kutoka Australia katika kategoria ya umri wa miaka 40 hadi 44.




Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kakamega, Kisumu na Eldoret.

Ili kupata habarizaidi tembelea tovuti ya radiojambo.