Msimu wa ligi kuu ya Kenya 2026/27 unaendelea leo, Ulinzi Star ikiwakaribisha Tusker katika uwanja wa Ulinzi jioni. Mechi hiyo itaanza saa nane mchana, kabla ya kufungua njia kwa AFC Leopards dhidi ya Bandari katika uwanja huo huo kuanzia saa 4.15 alasiri. Wakati huo huo, timu mpya ya 3K FC itapambana na Mara Sugar katika uwanja wa Embu, huku timu nyingine mpya ya Migori Youth ikiikaribisha Police FC katika uwanja wa Awendo kabla ya Mombasa United kupambana na Kakamega Homeboyz.
Jua linashuhudiwa Meru, Isiolo na Mrasabit.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.