Rais William Ruto amewahimiza Wakenya kuendeleza juhudi za uhifadhi wa mazingira huku nchi ikilenga kupanda miti bilioni 15 ifikapo mwaka 2032 ili kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kurejesha misitu. Rais aliongoza taifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira huko Endebess, Kaunti ya Trans Nzoia, ambapo alisambaza miche ya kakao kwa wakulima, akiashiria mwanzo wa kupanda zao hilo nchini ili kukuza zao hilo kama chanzo cha mapato na ulinzi wa mazingira.

WILLIAM RUTO-TREES