Mamlaka ya Mapato nchini imetangaza kufungwa kwa mfumo wake wa iSCAN kwa saa 12 leo ili kurahisisha matengenezo yaliyopangwa. Katika notisi, mamlaka hiyo ilisema mfumo huo hautapatikana kwa watumiaji wote kuanzia saa kumi alfajiri hadi saakumi jioni, na hivyo kuvuruga kwa muda upatikanaji wa huduma zinazotolewa kupitia mfumo huo. KRA imewasihi wadau kupanga ipasavyo na kuomba radhi kwa usumbufu wowote uliosababishwa.