Ligi Kuu ya Kenya inaanza kesho huku Mathare United ikipambana na APS Bomet katika uwanja wa Police Sacco. Wakati huo huo, Posta Rangers watapambana na Shbana katika uwanja wa Wanguru wakiwa na pointi tatu za kung'ang'ania. Kesho, Ulinzi stars watawakaribisha Tusker katika uwanja wa Ulinzi huku wageni 3K FC wakipambana na Mara Sugar katika uwanja wa Embu, huku mgeni mwingine Migori Youth akicheza na Police FC katika uwanja wa Awendo, nayo Mombasa United ikiwakaribisha Kakamega Homeboyz.


AFC Leopards watakamilisha mechi za Jumapili dhidi ya Bandari katika uwanja wa Ulinzi. Wakati huo huo, mabingwa Gor Mahia watacheza dhidi ya Muranga Seals Jumanne katika uwanja wa Nyayo saa moja usiku.



 Jua linashuhudiwa Makindu, Mtito andei na Voi.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.