Shirika la Afya Duniani limesifu Kenya kwa hatua yake ya haraka ya kukabiliana na kisa cha kwanza cha Ebola nchini. Akizungumza katika Afya House wakati wa hafla ya kukabidhi awamu ya kwanza ya vifaa vya maabara na vifaa muhimu vya kujikinga vyenye thamani ya Shilingi milioni 2.97, Mwakilishi wa WHO, Neema Kimambo, aliahidi kuendelea kutolewa msaada kwa juhudi za kudhibiti ugonjwa huo na kuhakikisha usalama wa umma.
NEEMA KIMAMBO – WHO