Wazazi wametakiwa kuchukua hatua mapema wanapoona mabadiliko ya kihisia au kitabia kwa watoto wao, kwani hii inaweza kuashiria matatizo ya afya ya akili yaliyojificha. Mwanasaikolojia wa watoto, Florence Ochanda, anasema kuwa kubaini tatizo mapema huwapa wazazi fursa ya kutafuta msaada wa kitaalamu na kuzuia tatizo hilo kuwa kubwa zaidi. Anaongeza kuwa hali kama hizo zinaweza kudhibitiwa baada ya kufanyiwa tathmini sahihi ya kimatibabu.
FLORENCE OCHANDA - SIGNS