Zaidi ya wakaazi 3,000 wa Embobut, Marakwet Mashariki, Kaunti ya Elgeyo-Marakwet, wametia saini tamko la kuachana na desturi ya Ukeketaji wa Wanawake na badala yake kulinda na kuwawezesha wasichana. Wakaazi hao walitoa ahadi hiyo katika hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya St. Michael huko Embobut, wakiahidi kushirikiana na viongozi wa jamii pamoja na wadau wengine kutokomeza desturi hiyo. Mwakilishi wa vijana, Sonita Sonaiya, alisema tamko hilo ni hatua muhimu katika kuwalinda wasichana na kukuza elimu yao.