Wahadhiri wa vyuo vikuu wamekaribisha mazungumzo kuhusu mzozo wao wa mishahara, lakini wanasema ni lazima serikali kwanza ilipe Shilingi bilioni 100 za malimbikizi ya malipo yao kabla hawajasitisha mgomo wao. Katibu Mkuu wa UASU, Constantine Wasonga, anasema wahadhiri wako tayari kurejea mezani kwa mazungumzo iwapo matakwa yao yatatimizwa. Pia wanataka kuajiriwa kwa wahadhiri elfu 25 katika vyuo vikuu vya umma na kutekelezwa kwa makubaliano kuhusu fedha za kustaafu.
WASONGA NYONGESA - PROMOTION