Viongozi wa biashara na sekta wanatoa wito wa mwitikio ulioratibiwa wa umma na binafsi kufuatia kuthibitishwa kwa kisa cha kwanza cha Ebola nchini Kenya. Wakiongozwa na mwenyekiti wa Chama cha vituo vya Petroli cha Kenya, Martin Chomba, viongozi hao walionya kwamba kushindwa kudhibiti ugonjwa huo kunaweza kudhoofisha imani ya utalii na wawekezaji. Chomba alisema mkurupuko huo unaweza pia kuwaweka Wakenya wanaosafiri nje ya nchi katika hatua za ziada za uchunguzi na karantini kabla ya kuingia katika nchi zingine, na hivyo kuvuruga usafiri wa kimataifa na biashara.

MARTIN CHOMBA - EBOLA