Nchi ya Uchina imeipa Kenya ruzuku ya Sh milioni 260 ili kuimarisha mwitikio wa nchi hii dhidi ya ukame na maandalizi ya mkurupuko wa Ebola. Chini ya ruzuku hiyo, Shmilioni 130 zitasaidia juhudi za kupunguza ukame, huku Sh milioni 130 nyingine zitaimarisha utayari na mwitikio wa Kenya dhidi ya mkurupuko wa Ebola. Balozi wa Uchina nchini Kenya Guo Haiyan alikabidhi rasmi ruzuku hiyo kwa serikali ya Kenya katika Hazina ya Kitaifa.