Rais William Ruto ametetea uamuzi wa serikali yake wa kutumia rasilimali za taifa kuvutia uwekezaji, huku akipinga madai ya upinzani kwamba mkakati huo ni sawa na kuuza rasilimali muhimu za nchi. Ruto alisema fedha zinazotokana na rasilimali zilizobinafsishwa zinasaidia kuendeleza miundombinu nchini bila kuhitaji mikopo. Alisisitiza kuwa kampuni zilizofanyiwa mageuzi ya kibiashara au kubinafsishwa zinaendelea kufanya kazi nchini Kenya, akionyesha kuwa nchi haijapoteza rasilimali hizo.
WILLIAM RUTO - PESA