Polisi wanachunguza vifo vya wanaume wawili ambao miili yao ilipatikana ikielea katika Mto Migori, eneo la Matanda katika Kaunti Ndogo ya Nyatike. Polisi walisema kuwa miili ya Michael Onyango, mwenye umri wa miaka 50, na Charles Owino, mwenye umri wa miaka 41, iligunduliwa Jumanne. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa wanaume hao wawili walionekana kwa mara ya mwisho wakiwa pamoja huko Matanda saa mbili usiku, Jumatatu. Polisi wanashuku kuwa huenda walizama walipokuwa wakijaribu kuvuka Mto Migori kuelekea eneo la Ogaka.