Kiongozi wa chama cha UGM, David Maraga, ameishutumu serikali ya Rais William Ruto kwa kusimamia uharibifu mkubwa wa misitu na mifumo muhimu ya ikolojia nchini. Maraga alikosoa uamuzi wa serikali wa kuondoa marufuku ya ukataji miti, akisema hatua hiyo imeiacha misitu iliyohifadhiwa na maeneo ya vyanzo vya maji katika hatari ya kuharibiwa zaidi. Jaji Mkuu huyo wa zamani alisema serikali inapaswa kuchukulia uhifadhi wa mazingira kama uwekezaji wa kiuchumi badala ya kikwazo kwa shughuli za kibiashara.