Kamishna wa Kaunti ya Kirinyaga, Shufaa Mwijuma, amewataka vijana kushirikiana na serikali katika vita dhidi ya pombe haramu na dawa za kulevya, akisisitiza kuwa ushirikishwaji wa jamii ni muhimu katika kukabiliana na tatizo hilo. Mwijuma alisema serikali imebadili mwelekeo kutoka kwenye operesheni za kawaida za msako na ukaguzi na kuanza kuwashirikisha vijana moja kwa moja ili kuelewa changamoto zinazowasukuma katika matumizi mabaya ya pombe na dawa za kulevya.