Shirika la UNICEF limepanga kuwachunguza karibu watoto elfu 50 katika kaunti za Vihiga na Isiolo kwa magonjwa manne yasiyo ya kuambukiza chini ya mpango wa miaka mitatu. Mpango huo utawalenga watoto wenye umri wa miaka sifuri hadi 19 na kuzingatia Kisukari cha type 1, ugonjwa wa seli mundu, pumu na magonjwa ya moyo. Mratibu wa Magonjwa Yasiyo ya kuambukiza wa Kaunti ya Vihiga, Mike Olonyo, alisema mpango huo unalenga kugundua hali hizo mapema na kuwaunganisha watoto walioathiriwa na huduma inayofaa. Afisa wa Kliniki, Sophie Omutere, alisema kugundua mapema na usimamizi sahihi kunaweza kuboresha maisha ya watoto wanaoishi na magonjwa haya.