Waziri wa ICT William Kabogo anasema serikali imeimarisha hatua za kisheria, kitaasisi na kiufundi ili kukabiliana na vitisho vya mtandaoni nchini. Kabogo anasema Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya hufuatilia mazingira ya mtandaoni na kuratibu hatua za kukabiliana na matukio ya watu kujifanya ni maafisa au taasisi za serikali, wizi wa taarifa nyeti, na mawasiliano yenye kuchochea vurugu. Anaongeza kuwa Kamati ya Kitaifa ya Uratibu wa Masuala ya Kompyuta na Mtandao huleta pamoja taasisi za serikali, vyombo vya kutekeleza sheria, wadhibiti, na sekta za miundombinu muhimu ili kubadilishana taarifa na kuratibu hatua za kukabiliana na changamoto hizo.
WILLIAM KABOGO – THREATS