Imani na desturi za kidini haziwezi kutumika kuwazuia watoto kupata elimu ya msingi. Waziri wa Elimu Julius Ogamba anasema Wizara hiyo itatekeleza sera ya mpito ya asilimia 100 huku ikilinda uhuru wa kikatiba wa dhamiri, dini, imani na maoni ya wanafunzi. Anasema shule lazima zitoe nafasi za ibada na hazipaswi kuwalazimisha wanafunzi kushiriki katika shughuli za kidini kinyume na imani zao, akionya kwamba ukiukaji huo utasababisha hatua za kisheria.
JULIUS OGAMBA – DISCRIMINATION