Mimba za utotoni zinaweza kuwaweka wasichana katika hatari ya matatizo makubwa ya kiafya, ikiwemo uchungu wa mapema, fistula na majeraha katika njia ya uzazi. Mwanagainakolojia, Weston Khisa, anasema kuwa wasichana wengi hawajakomaa kikamilifu kimwili, jambo linalowaweka katika hatari kubwa zaidi ya matatizo kama vile shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito na upungufu wa damu mwilini. Anaongeza kuwa msongo wa mawazo unaotokana na ujauzito katika umri mdogo unaweza pia kusababisha kiwewe.
WESTON KHISA – PREGNANCY