Misa ya wafu kwa ajili ya mahujaji 17 Wakatoliki kutoka Parokia ya Katoliki ya St Mathias Mulumba huko Mikindani, Kaunti ya Mombasa, waliofariki katika ajali ya barabarani walipokuwa wakisafiri kwenda Subukia kwa ajili ya Siku ya Maombi ya Kitaifa, itafanyika leo huku familia zikijiandaa kuwapumzisha wapendwa wao. Misa hiyo imepangwa kuanza saa nne asubuhi katika parokia hiyo, huku jamaa, marafiki na waumini wenza wakitarajiwa kukusanyika ili kuwaenzi marehemu na kuwaombea roho za wale waliopoteza maisha yao katika msiba huo.
ABANEAS BARASA- FINAL CALL