Waziri wa Elimu Julius Ogamba anasema kuwa kwa sasa Wizara ya Elimu haina takwimu za kina na zilizogawanywa kulingana na makundi mbalimbali kuhusu idadi ya wasichana walio na na watoto ambao wamerejea shuleni au wale ambao bado hawajarejea. Waziri Ogamba anasema pengo hili litashughulikiwa kupitia Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu nchini Kenya (KEMIS), ambao umebuniwa kukusanya taarifa kuhusu kurejea shuleni. Mfumo huo unatarajiwa kutoa taarifa zilizo wazi zaidi kuhusu upatikanaji wa elimu kwa akina mama wenye umri wa ujana.

JULIUS OGAMBA – TEENAGE MOTHERS