Waziri wa Afya Aden Duale anatarajiwa kukutana leo na wanadiplomasia ili kuwapa taarifa kuhusu hatua za Kenya za kukabiliana na kudhibiti hali, kufuatia kisa cha kwanza cha Ebola kuripotiwa nchini. Duale alisema mkutano huo unalenga kuwahakikishia wanadiplomasia usalama na kuzuia kutolewa kwa tahadhari za usafiri zinazoweza kuathiri sekta ya utalii. Alisisitiza kuwa hakuna sababu ya hofu, akibaini kuwa kisa hicho kiliingizwa kutoka nje, lakini akawataka wananchi kuwa waangalifu ili kuzuia maambukizi zaidi.

ADEN DUALE - ALERTS