Mbunge wa EALA Winnie Odinga anasema urithi wa marehemu babake hauwezi kusimuliwa bila kuwatambua Wakenya wa kawaida waliosimama naye katika safari yake yote ya kisiasa. Akizungumza huko Bondo, Winnie alisema wafuasi wengi wa Raila hawakuwa na vyeo au fursa ya kukutana na viongozi wa kisiasa, lakini walisafiri umbali mrefu, walisimama kwenye mvua na waliamini Kenya inaweza kuwa bora zaidi. Aliwaalika Wakenya kuheshimu kumbukumbu yake kupitia nyimbo, densi, mashairi na kumbukumbu za kibinafsi.
WINNIE ODINGA – RAILA