Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi amewataka wakosoaji wanaoulizia kuhusu mradi uliopendekezwa wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha Lamu kuwasilisha hoja zao kwake, akisema Wizara ya Nishati ndiyo inayohusika na mradi huo. Wandayi alisema atajibu maswali yanayohusu mradi huo, ikiwemo hoja kuhusu mikataba inayohusiana na kiwanda hicho. Akizungumza na wanahabari jijini Kisumu, Waziri huyo alisema wakosoaji wanapaswa kuacha kumtumia Rais William Ruto kama ngao wanapoulizia maamuzi yanayohusu wizara yake.
OPIYO WANDAYI – OBSESSION