Serikali imewasihi wahudumu wa afya kuendelea kuwa macho na kufuata kwa makini hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi baada ya kuthibitishwa kwa kisa cha Ebola nchini Kenya. Wakenya pia wameshauriwa kutafuta matibabu katika vituo vya afya vinavyotambulika ikiwa wanahisi vibaya. Waziri wa Afya Aden Duale pia ametoa wito kwa umma kuripoti mtu yeyote anayeonyesha dalili za ugonjwa huo kwa kituo cha afya kilicho karibu ili kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
ADEN DUALE -VIGILANT