Rais William Ruto leo ataongoza hafla ya kuweka wakfu na kuzindua rasmi kaburi maalum (mausoleum) la marehemu Raila Odinga huko Kang’o Ka Jaramogi, Bondo. Hafla hiyo inafanyika katika mwezi uliotengwa kwa ajili ya kukumbuka na kuenzi maisha, urithi, na mchango wa Raila, huku taifa likiadhimisha mwaka mmoja tangu kifo chake. Waziri wa Jinsia Hanna Cheptumo, alisema kuwa kaburi hilo litatoa mahali ambapo vizazi vijavyo vitaweza kujifunza kuhusu maisha ya Raila na kuelewa muktadha wa kihistoria wa kipindi alichoishi na kutumikia.