Kenya imeongeza ufuatiliaji katika vituo rasmi vya mpakani na kuimarisha uchunguzi wa wasafiri kufuatia uthibitisho wa kisa cha kwanza cha ugonjwa wa virusi vya Ebola vYA Bundibugyo nchini humU. Mkurugenzi Mkuu wa Afya Patrick Amoth anasema Wizara ya Afya itaendeleza ufuatiliaji wa hali ya juu katika vituo vya mpakani, ikiwa ni pamoja na Busia na Malaba, huku mamlaka zikichukua hatua za kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo.

PATRICK AMOTH – EBOLA