Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma amepinga ombi la dhamana kwa watu saba wanaokabiliwa na mashtaka ya mauaji ya daktari wa magonjwa ya akili, Victoria Mutiso. Waendesha mashtaka walimweleza Jaji Alexander Muteti kuwa kuwaachilia huru washitakiwa hao kunaweza kuhatarisha usalama wa mashahidi na familia zao, kwa kuwafanya wakabiliwe na vitisho au uingiliaji kati, na pia kunaweza kuhujumu uchunguzi unaoendelea pamoja na kesi yenyewe. Washitakiwa hao saba, ambao wamekana mashtaka, wanadaiwa kushirikiana kumuua Mutiso mnamo tarehe 29 Julai eneo la Kilimani.

 

JALSON MAKORI – OPPOSE