Waziri wa Mazingira Deborah Barasa anasema wazee wa kijiji watachukua jukumu muhimu katika kuandaa jamii kwa ajili ya hali inayotarajiwa ya El Niño. Barasa anasema zaidi ya wazee wa kijiji elfu 108 watakuwa na taarifa za kusaidia jamii kuepuka uchafuzi wa mazingira, kurejesha mifumo ikolojia na kujiandaa kwa mafuriko na maporomoko ya ardhi. Anasema wale wanaoishi kando ya mito na katika maeneo yanayokumbwa na maporomoko ya ardhi watashauriwa kuhamia maeneo salama zaidi kama sehemu ya kujiandaa na maafa.
DEBORAH BARASA – ROLE