Katibu wa Wizara ya Mambo ya kigeni, Korir Sing’Oei, ametoa wito wa kufanyiwa marekebisho kwa mifumo ya kifedha ya kimataifa, akisema kuwa inaendelea kuwa na athari mbaya kwa nchi za Afrika. Akizungumza jijini Paris, Sing’Oei alisema kuwa mataifa ya Afrika hulipa gharama kubwa zaidi—mara tatu hadi nne—kupata mitaji ikilinganishwa na nchi za Ulaya, huku gharama za kukopa zikipanda kwa asilimia 91 kati ya mwaka 2020 na 2024. Alizitaka nchi zenye nguvu duniani kukuza mifumo ya kifedha ya haki, upatikanaji halisi wa masoko, na uhuru wa biashara unaounga mkono juhudi za Afrika za kujiendeleza kiviwanda.