Waziri wa Elimu Julius Ogamba amesisitiza tena ahadi ya serikali ya kuboresha maslahi ya walimu kupitia malipo ya mishahara kwa wakati, kupandishwa vyeo kwa haki, njia wazi za maendeleo ya kitaaluma na uimarishaji endelevu wa uwezo wao. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani jana, Ogamba alisema kuwa kuongeza uwekezaji na kuajiri walimu zaidi ni muhimu sana katika kuimarisha sekta ya elimu. Pia aliwapongeza walimu kwa mchango wao katika kutekeleza mfumo wa elimu wa CBE na kuhimiza ushirikiano zaidi kati ya walimu, wazazi na jamii.

 

JULIUS OGAMBA – COMMITMENT