Serikali imenunua chini ya gunia milioni moja za mahindi kutoka kwa wakulima wa humu nchini katika juhudi za kuziba pengo la upungufu wa gunia milioni 25. Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe anasema Kenya itaagiza mahindi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na COMESA ili kudumisha usambazaji wa kutosha. Akizungumza na NTV, Kagwe alisema upungufu huo hausababishi dharura, huku uagizaji wa mahindi ukitarajiwa kuhakikisha kuna mtiririko endelevu wa mahindi sokoni.

MUTAHI KAGWE-MAIZE