Tume ya Masuala ya Jinsia imesema itashirikiana na Tume ya IEBC kuhakikisha kuwa vituo vya kupigia kura vinafikika kwa urahisi na watu wenye ulemavu pamoja na wazee kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Mwenyekiti Rehema Jaldesa, alithibitisha hayo wakati wa mkutano na Serikali ya Kaunti ya Turkana mjini Lodwar. Vilevile, Jaldesa aliomba uungwaji mkono kutoka kwa kaunti hiyo kwa ajili ya pendekezo la kuanzisha ofisi ya kikanda ya tume ya jinsia mjini Lodwar ili kuboresha uwezo wa Tume hiyo kuwafikia wananchi.