Sekta ya utalii nchini Kenya inajiandaa kwa maonyesho makubwa zaidi ya *Magical Kenya Travel Expo* kuwahi kufanyika, huku maelfu ya wataalamu wa utalii wakitarajiwa jijini Nairobi wakati nchi ikijitahidi kuimarisha uwepo wake katika masoko ya kimataifa na kukuza biashara inayotokana na wageni. Toleo la 16 la maonyesho hayo linaanza leo katika bustani ya Uhuru Gardens, likikutanisha wanunuzi wa kimataifa, waonyeshaji, mashirika ya utalii, mashirika ya ndege, hoteli, waendeshaji wa ziara, kampuni za teknolojia na wadau wengine kutoka nyanja mbalimbali za sekta ya usafiri na utalii. Waandaaji wanatarajia zaidi ya wajumbe elfu 10 kutoka nchi 40 na zaidi ya waonyeshaji 400.
JUNE CHEPKEMOI – EXPO