Shirika la Msalaba Mwekundu nchini limesema kuwa lori la kubeba mafuta lililipuka muda mfupi baada ya saa sita usiku eneo la Sachangwan, kwenye sehemu ya barabara kuu ya Nakuru-Eldoret iliyo kati ya Salgaa na Nakuru. Shirika hilo limeeleza kuwa timu yake ilifika eneo la tukio na kuwahudumia watu wawili walioathirika. Tukio hilo limesababisha kufungwa kwa barabara kuu katika makutano ya Kibunja na Soilo. Shirika hilo limewataka madereva wanaotumia barabara hiyo kutumia njia mbadala huku shughuli za kutatu tukio hilo zikiendelea.