Waziri wa Mazingira Deborah Barasa anasema kuwa kuregeshwa kwa mfumo ikolojia kunapaswa kuchukuliwa kama fursa ya kiuchumi badala ya shughuli ya kimazingira pekee. Barasa anasema miche milioni 17 inayolengwa kupandwa wakati wa shughuli za Siku ya Mazingira itachangia katika uchumi wa kijani na kuunda fursa za kiuchumi. Anasema wakulima wanaweza kunufaika kupitia kilimo-misitu, huku kampuni binafsi na washirika wa maendeleo wakihimizwa kuwekeza katika shughuli za urejeshaji na uchumi wa kijani kote nchini Kenya.

DEBORAH BARASA – TREES