Taasisi ya kuunda Mitaala nchini (KICD) imetoa vitabu vya kiada na vitabu vya fasihi vilivyoidhinishwa kwa ajili ya Grade ya 11 na kuanza kuvigawa katika shule za kawaida na zile za Elimu Maalum, kabla ya wanafunzi wa Grade ya 10 kuhamia darasa hilo mnamo Januari mwaka ujao. Orodha kamili inapatikana katika 'Orange Book' kwenye tovuti ya KICD, huku miundo ya mitaala iliyoidhinishwa ikipatikana katika maduka ya vitabu ya KICD na mtandaoni. KICD imesema kuwa zoezi la ugawaji litafanyika kuanzia leo hadi tarehe 23 Oktoba kabla ya kusitishwa kwa muda ili kupisha mitihani na tathmini za kitaifa.