Gavana wa Trans Nzoia, George Natembeya, ameahidi kutoa Shilingi milioni 5 kusaidia utengenezaji wa viungo bandia na vifaa vingine vya kusaidia watu wenye ulemavu katika Hospitali ya Kaunti ya Kitale. Pia, Natembeya alitoa Shilingi milioni 2 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya kuendeleza uzalishaji wa vifaa hivyo. Akizungumza wakati wa ziara yake katika hospitali hiyo, gavana huyo alisema kuwa kaunti hiyo itawaunga mkono watu wenye ulemavu ili waweze kupata vifaa vinavyoboresha hali yao ya maisha.

GEORGE NATEMBEYA - REKEBISHA