Gavana wa Nairobi Johnson Sakaja ametoa wito kwa wakaazi kusafisha mazingira yao ili kusaidia kaunti kujiandaa kwa mvua ijayo ya El Niño. Akizungumza huko Kasarani alipokuwa akiongoza usafi wa mitaro ya maji katika kaunti zote ndogo 17, alisema Nairobi itakuwa tayari mvua itakapofika katika wiki mbili. Zaidi ya wafanyakazi 4,500 wa Green Army wanasafisha mitaa, barabara na maeneo ya umma, na kuharakisha ukusanyaji wa taka.
JOHNSON SAKAJA - MAZINGIRA