Maafisa wa upelelezi huko Githurai, Kaunti ya Kiambu, wanachunguza kisa cha kuuawa kwa mwanamume wa umri wa makamo ambaye hajafahamika, aliyedungwa kisu wakati wa ugomvi uliotokana na suala la simu ya mkononi. Polisi na mwalioshuhudia walisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumamosi, majira ya saa sita na nusu usiku, katika Eneo la Githurai. Wanaume hao wawili walionekana wakitembea kando ya jengo hilo huku wakizozana kabla ya kuanza kupigana.