Mwanamume mmoja alikamatwa baada ya kudaiwa kujaribu kuingia kwa nguvu katika eneo lenye ulinzi mkali la Ikulu kupitia Lango D jijini Nairobi mnamo alasiri ya Jumapili. Tukio hilo liliripotiwa mwendo wa saa 1:32 mchana baada ya maafisa wa usalama wa kikosi cha GSU waliokuwa wakilinda lango hilo kugundua mwanamume akijaribu kuingia katika eneo hilo. Polisi walisema mshukiwa alikuwa akiendesha tuk-tuk wakati alipodaiwa kujaribu kuingia kwa nguvu kupitia Lango D.