Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Isiolo, Mumina Bonaya, anawataka viongozi kutoka jamii za wafugaji kuchagua njia ya mazungumzo na kuacha vitendo vya uhalifu wa kutumia silaha na wizi wa mifugo ili kudumisha amani ya kudumu. Akizungumza katika kongamano la kuimarisha amani huko Oldonyiro, Bonaya alisisitiza kuwa mijadala kuhusu uhalifu huo lazima iweke kipaumbele maisha ya binadamu, wajane, na yatima badala ya kuzingatia tu mifugo iliyoibiwa. 

MUMINA BONAYA - VITA