Mke wa Rais, Mama Rachel Ruto, amewapongeza walimu kote nchini kwa mchango wao katika kuwalea watoto, kukuza uwezo wao na kuwaandaa kuwa raia wenye uwajibikaji. Katika ujumbe wake wa kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani, Rachel alisema walimu wana jukumu muhimu katika kuwasaidia watoto kugundua vipaji vyao na kujenga kujiamini.