Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, amepuuza matokeo ya hivi karibuni ya tafiti za maoni zinazoonyesha kuwa Rais William Ruto anafurahia uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa umma, akisisitiza kuwa hawezi kupata zaidi ya asilimia 10 katika utafiti wowote wa kuaminika. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa chama cha 'The Equitable Party', Khalwale alihoji uhalali wa tafiti zinazompa Ruto uungwaji mkono wa asilimia 45. Alisema kuwa tafiti za aina hiyo zinaweza kutumika kupotosha mtazamo wa umma kuelekea uchaguzi.

BONI KHALWALE - RESULTS