Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale, amemuonya Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kuwa hatua ngumu zaidi ya azma yake ya kuwania urais ndiyo kwanza imeanza. Akizungumza katika hafla ya kuzindua chama cha Sifuna, 'Equitable Party', jijini Nairobi, Khalwale alisema sifa binafsi pekee hazitoshi kumwezesha mtu kushinda urais. Alimtaka Sifuna kuwatafuta viongozi wakuu wa upinzani na kujipatia uungwaji mkono kutoka kwa wanasiasa wenye uzoefu mkubwa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
BONI KHALWALE - STAND