Kiongozi wa DCP, Rigathi Gachagua, amemsifu Seneta wa Nairobi, Edwin Sifuna, kwa kuzindua chama chake kipya, akisema hatua hiyo ni mwanzo wa safari yake kuelekea uongozi wa kitaifa. Gachagua alimtaka Sifuna kuchukua hatua za haraka kukijenga chama hicho na kutafuta wagombea imara katika maeneo ambayo ana nguvu kubwa kisiasa. Alisema upinzani unahitaji kuwa na idadi kubwa ya wabunge katika mabunge yote mawili ili kufanikisha ajenda zake za kisheria, huku akiishutumu serikali ya Ruto kwa kudhoofisha nchi.