Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amethibitisha azimio la serikali la kurejesha amani ya kudumu katika Bonde la Kerio lenye utata. Akizungumza huko Eldoret, alisema shughuli za usalama dhidi ya wahalifu zimeimarishwa na zitaendelea hadi usalama utakaporejea kikamilifu. Lagat aliongeza kuwa maafisa pia wanayakandamiza magenge ya wahalifu kote Kaskazini mwa Bonde la Ufa na sehemu za Magharibi mwa Kenya, wakiwalinda wakaazi huku nchi ikikaribia uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

ELIUD LAGAT - EXTEND