Wahadhiri wametetea mgomo wao, wakiishutumu serikali kwa kuchelewesha mazungumzo na utekelezaji wa CBA ya mwaka 2025–29. Akizungumza katika kipindi cha asubuhi cha NTV, Katibu Mkuu wa KUSU, Charles Mukhwaya, alisema mazungumzo hayo hayakuleta mwafaka licha ya chama hicho kuwa tayari kushiriki. Aliishutumu serikali kwa kutupia lawama taasisi zake kuhusiana na kuchelewa kwa mazungumzo na utekelezaji wa makubaliano hayo.

CHARLES MUKHWANA-CBA