Seneta wa Machakos, Agnes Kavindu, ameiomba Kamati ya Afya ya Seneti kuandaa mpango madhubuti wa kudhibiti wanyama wanaozurura na kuhakikisha upatikanaji wa chanjo. Akirejelea tukio la mwezi Agosti huko Syokimau ambapo kijana mmoja alijeruhiwa vibaya na mbwa, Kavindu alionya kuhusu kuongezeka kwa hatari ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa, akisisitiza haja ya hatua za haraka kuchukuliwa ili kulinda jamii dhidi ya mbwa wanaozurura katika maeneo ya makaazi.

AGNES KAVINDU - STRAY